Galatians 2:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambao waonekana kuwa viongozi wakuu, walitambua kwamba Mungu alinijalia neema hiyo, wakatushika sisi mkono, yaani Barnaba na mimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasa tukafanye kazi kati ya watu wa mataifa mengine, na wao kati ya Wayahudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yakobo, Kefa na Yohana, walioonekana kama nguzo za jumuiya ya waumini, walitupatia mkono wa shirika, mimi na Barnaba, walipotambua ile neema niliyopewa. Wakakubali kwamba sisi twende kwa watu wa Mataifa, na wao waende kwa Wayahudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yakobo, Petro na Yohana walikuwa viongozi muhimu kanisani. Hawa wakaona kuwa Mungu alinipa kipaji hiki maalumu cha huduma, hivyo wakatupa mkono wa shirika mimi pamoja na Barnaba. Wakakubali kuwa sisi tutaendelea kufanya kazi miongoni mwao wasio Wayahudi, na wao wataendelea kufanya kazi miongoni mwao walio Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambao waonekana kuwa viongozi wakuu, walitambua kwamba Mungu alinijalia neema hiyo, wakatushika sisi mkono, yaani Barnaba na mimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasa tukafanye kazi kati ya watu wa mataifa mengine, na wao kati ya Wayahudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambao waonekana kuwa viongozi wakuu, walitambua kwamba Mungu alinijalia neema hiyo, wakatushika sisi mkono, yaani Barnaba na mimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasa tukafanye kazi kati ya watu wa mataifa mengine, na wao kati ya Wayahudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, walioonekana kama nguzo za kanisa, walitupa mkono wa shirika, mimi na Barnaba walipotambua ile neema niliyopewa. Wakakubali kwamba sisi tuende kwa watu Mataifa na wao waende kwa Wayahudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, walioonekana kama nguzo za jumuiya ya waumini, walitupa mkono wa shirika, mimi na Barnaba, walipotambua ile neema niliyopewa. Wakakubali kwamba sisi twende kwa watu wa Mataifa, na wao waende kwa Wayahudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena Yakobo, Kefa, na Yohana, waliosifika kuwa ni nguzo, walipoitambua ile neema niliyopewa, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kulia wa kuonesha ushirikiano; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambao waonekana kuwa viongozi wakuu, walitambua kwamba Mungu alinijalia neema hiyo, wakatushika sisi mkono, yaani Barnaba na mimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasa tukafanye kazi kati ya watu wa mataifa mengine, na wao kati ya Wayahudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokitambua kipaji, nilichogawiwa, ndipo, Yakobo na Kefa na Yohana wanaowaziwa kuwa nguzo walipotupa mimi na Barnaba mikono kwamba: Tu mmoja, sisi tuipige hiyo mbiu kwao wamizimu, lakini wao kwao waliotahiriwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Yakobo, Petro na Yoane, waliohesabiwa kuwa waongozi wakubwa, walitambua neema ile niliyojaliwa na Mungu wakatupatia mukono, mimi na Barnaba kuwa kitambulisho cha ushirika. Hivi tukapatana kwamba sisi tutakwenda kuhubiri watu wa mataifa mengine na wao watakwenda kuhubiri Wayuda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;