Galatians 3:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: “Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, yuko chini ya laana.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya Torati wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Torati.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini watu wale wanaodhani kuwa kutii sheria ndicho kitu muhimu sana daima hukaa chini ya tishio la laana. Kama vile Maandiko yanavyosema, “Amelaaniwa mtu yeyote atakayeacha kuzishika na kuzitii sheria hizi zote.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na Sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: “Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria, yuko chini ya laana.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: “Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, yuko chini ya laana.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria, wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa mtu yule asiyeshika na kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Torati.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: “Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, yuko chini ya laana.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wote walio wenye kuyafanya Maonyo hawajatoka bado kwenye kuapizwa. Kwani imeandikwa: Na awe ameapizwa kila mtu asiyeandamana nayo yote yaliyoandikwa katika chuo cha Maonyo, ayafanye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wale wanaotegemea kutimiza yale yanayoamuriwa na Sheria, wamelaaniwa. Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Alaaniwe mutu yeyote asiyedumu katika yote yanayoandikwa katika hiki kitabu cha Sheria na kuyatii.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.