Galatians 3:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Al-Masihi alitukomboa kutoka laana ya Torati kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria inasema kuwa sisi Wayahudi tuko chini ya laana kwa kutokuitii daima. Lakini Kristo alituweka huru kutoka katika laana hiyo. Alikubali kulaaniwa na sheria ili atuokoe. Maandiko yanasema, “Yeyote anayening'inizwa mtini yuko chini ya laana.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya Sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Al-Masihi alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kristo alitukomboa, tusiapizwe na Maonyo, alipoapizwa kwa ajili yetu, kwani imeandikwa: Kila aliyetundikwa mtini ameapizwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kristo alitukomboa toka laana ya Sheria, akijitwalia laana hiyo kwa ajili yetu. Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Mutu yeyote anayetundikwa juu ya muti amelaaniwa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti: