Galatians 3:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uhai, basi, tungeweza kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je basi, Torati inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama Torati iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kupitia kwa Torati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, hili lamaanisha kwamba sheria hutenda kazi kinyume na ahadi za Mungu? La hasha. Sheria iliyotolewa kamwe haikuwa na uwezo wa kuwaletea watu maisha mapya. Ingekuwa hivyo, basi tungehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kuifuata sheria.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, Sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi, tungeweza kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uhai, basi, tungeweza kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, hakika haki ingalipatikana kwa sheria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uhai, basi, tungeweza kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena je? Maonyo huvikataa viagio vya Mungu? La, sivyo! Kwani kama yangekuwako Maonyo yaliyotolewa kuwa yenye nguvu ya kuwapa watu uzima, wongofu ungepatikana kweli kwa kuyafanya maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ni kusema kwamba Sheria haipatani na ahadi za Mungu? Hapana, hata kidogo! Kama kungetolewa Sheria yenye uwezo wa kuleta uzima kwa watu, basi mutu angehesabiwa haki mbele ya Mungu kwa njia ya Sheria.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha. Kwa kuwa, kama ingalitolewa sharia iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sharia.