Galatians 3:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi aliyotoa Mungu, kwa kumwamini Yesu Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kupitia kwa imani katika Isa Al-Masihi yapate kupewa wale wanaoamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hilo halikuwa kusudi la sheria. Maandiko yanauweka ulimwengu wote chini ya udhibiti wa dhambi kama aina ya kifungo gerezani. Ili kile ambacho Mungu aliahidi kipokelewe kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Hii hutolewa kwa wale wanaomwamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, kwa kumwamini Yesu Kristo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi aliyotoa Mungu, kwa kumwamini Yesu Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo yapate kupewa wale wanaoamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Isa Al-Masihi yapate kupewa wale wanaoamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi aliyotoa Mungu, kwa kumwamini Yesu Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Maandiko yamewafunga wote pamoja kuwa watumwa wa makosa kwamba: Wote watakaomtegemea wapewe kile kiagio kitokacho kwenye kumtegemea Yesu Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Maandiko Matakatifu yanasema kwamba watu wote wako chini ya utumwa wa zambi, kusudi zawadi iliyoahidiwa na Mungu itolewe kwa wale wanaoamini kwa njia ya imani yao katika Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.