Galatians 3:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kabla ya kujaliwa imani, sheria ilitufanya wafungwa, tukingojea imani hiyo ifunuliwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya Torati, tumefungwa hadi ile imani ifunuliwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kabla ya aliye mwaminifu kuja, sheria ilituweka sisi kama wafungwa. Hatukuwa huru hadi imani hii inayokuja ilipofunuliwa kwetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kabla ya kujaliwa imani, Sheria ilitufanya wafungwa mpaka imani hiyo iliyokuwa inakuja ifunuliwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kabla ya kujaliwa imani, sheria ilitufanya wafungwa, tukingojea imani hiyo ifunuliwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kabla ya kujaliwa imani, sheria ilitufanya wafungwa, tukingojea imani hiyo ifunuliwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Lakini tegemeo lilipokuwa halijatokea bado, tulilindwa, tuyatii Maonyo, tukawa tumefungwa pamoja, tungoje, tegemeo litakapofunuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa imani ulipokuwa haujatokea, tulichungwa na Sheria, kama vile wafungwa, tukingojea mpaka imani ile ifunuliwe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kabla ya kuja imani tulikuwa tumewekwa chini ya sharia, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.