Galatians 3:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa, ndani ya Kristo haijalishi kama wewe u Myahudi au Myunani, mtumwa au huru, mwanaume au mwanamke. Wote mko sawa katika Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja katika kuungana na Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwake yeye hakuna tena Myuda na Mgriki, wala mtumwa na mwungwana, wala mume na mke, kwani ninyi nyote m mmoja kwa kuwa wake Kristo Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo hakuna tena umbalimbali kati ya Wayuda na watu wa mataifa mengine, kati ya watumwa na watu huru, mwanaume na mwanamuke; kwa maana ninyi wote ni mumoja katika kuungana kwenu na Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.