Galatians 3:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Injili na kuiamini?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, Mungu huwapa Roho wake Mtakatifu na kufanya miujiza kati yenu kwa sababu mnatii Torati, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, Mungu anawapa ninyi Roho na kutenda miujiza miongoni mwenu kwa kuwa mnaifuata sheria? Hapana sivyo! Mungu anawapa ninyi baraka hizi kwa njia ya ujumbe unaoleta imani katika kumwamini Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Habari Njema na kuiamini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Injili na kuiamini?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Injili na kuiamini?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilikuwaje? Aliyewapa Roho na kufanya yenye nguvu kwenu aliyafanyia kwamba: Mmeyafanya Maonyo? au kwamba: Mmeyategemea, mliyoyasikia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu aliwajaza Roho wake na kufanya miujiza kati yenu kwa sababu munashika Sheria au kwa sababu munasikia na kuamini Habari Njema?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, yeye awaruzukiae Roho na kufanya miujiza kati yenu, afanya hayo kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani?