Galatians 4:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nasema hivi: Mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lile nisemalo ni kwamba wakati wote mrithi bado ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ndiye mmiliki wa mali yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninalolisema ni hili: Wakati mrithi wa vyote alivyomiliki baba yake bado ni mdogo, hana tofauti yo yote na mtumwa. Haijalishi kuwa anamiliki vitu vyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lile nisemalo ni kwamba wakati wote mrithi akiwa bado ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ndiye mmiliki wa mali yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lile nisemalo ni kwamba wakati wote mrithi bado ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ndiye mmiliki wa mali yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ni bwana wa yote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nasema hivi: Mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nasema: Kibwana siku anapokuwa mchanga bado, hakuna, apitanacho na mtumwa, angawa ni bwana wa vyote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ninataka kusema hivi: mwana anayepaswa kurizi mali ya baba yake anatendewa kama mutumwa kwa muda wote anapokuwa angali mudogo, ijapokuwa yeye ndiye kweli mwenyeji wa mali yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
LAKINI nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ajapokuwa bwana wa yote;