Galatians 4:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyangoa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imeenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngeng’oa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ku wapi, basi, kule kujiita heri? Maana nawashuhudu kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling'oa macho yenu, mkanipa mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlikuwa na furaha sana wakati huo. Nini kimetokea kwa imani yenu ya awali kwamba mimi nilikuwa mtu niliyebarikiwa kipekee na Mungu? Naweza kusema bila shaka yoyote kwamba mngeliweza kufanya kitu chochote kunisaidia. Kama ingeliwezekana, mngeliyang'oa hata macho yenu na kunipa mimi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyang'oa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyang'oa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imekwenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngeng'oa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imekwenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngeng’oa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuko wapi, basi, kule kujiita heri? Maana nawashuhudia kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling'oa macho yenu, mkanipa mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyangoa macho yenu na kunipa mimi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yale mashangilio yenu sasa yako wapi? Kwani nawashuhudia ninyi kwamba: Kama ingaliwezekana, mngaliyang'oa hata macho yenu, mkanipa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ku wapi, basi, kule kujiita heri? Maana nawashuhudu kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling’oa macho yenu, mkanipa mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi mulikuwa wenye furaha. Sasa nini imewatokea? Kwa maana ninaweza kuwashuhudia kwamba mungeweza kuongoa hata macho yenu na kuyatoa kwangu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ku wapi, bassi, kule kujiita kheri? Maana nawashuhudia, kwamba, kama ingaliwezekana, mngaliugʼoa macho yenu, mkanipa mimi.