Galatians 4:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao watu wengine wanawahangaikia nyinyi, lakini nia yao si njema. Wanataka kuwatenganisha nami ili nyinyi muwahangaikie wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa njia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hawa wanajitahidi sana kuonesha kuvutiwa nanyi, lakini hiyo siyo nzuri kwenu. Wanataka kuwashawishi ninyi ili mtugeuke sisi na kuambatana nao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hao watu wengine wanawahangaikia ninyi, lakini nia zao si njema. Wanataka kuwatenganisha nami ili ninyi muwahangaikie wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao watu wengine wanawahangaikia nyinyi, lakini nia yao si njema. Wanataka kuwatenganisha nami ili nyinyi muwahangaikie wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa nia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao watu wengine wanawahangaikia nyinyi, lakini nia yao si njema. Wanataka kuwatenganisha nami ili nyinyi muwahangaikie wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanavyowahimiza, si vizuri, ila wanataka kuwatenganisha na sisi, mpate kujihimiza kuwatumikia wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa njia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu wanaonyesha kwamba wanawashugulikia, lakini nia yao si nzuri. Wao wanataka kuwatenganisha na mimi, kusudi mupate kushugulika nao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wao wawaonea uinyi shauku lakini si kwa vema bali wanataka kuwafungia mlango illi ninyi mwaonee wao shauku.