Galatians 4:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watoto wangu, kama vile mama mjamzito anavyotaabika wakati wa kujifungua, mimi nataabika tena kwa ajili yenu mpaka hapo hali yake Kristo itakapoundwa ndani yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara nyingine ninawaonea uchungu, ninatamani kwamba Al-Masihi aumbike ndani yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watoto wangu wadogo, nasikia uchungu tena kwa ajili yenu, kama mama anayejifungua. Nitaendelea kusikia uchungu huu mpaka watu watakapofikia kumwona Kristo wawatazamapo ninyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watoto wangu, kama vile mama mja mzito anavyotaabika wakati wa kujifungua, mimi nataabika tena kwa ajili yenu mpaka hapo hali yake Kristo itakapoundwa ndani yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watoto wangu, kama vile mama mjamzito anavyotaabika wakati wa kujifungua, mimi nataabika tena kwa ajili yenu mpaka hapo hali yake Kristo itakapoundwa ndani yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara nyingine ninawaonea utungu, ninatamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara nyingine ninawaonea utungu, ninatamani kwamba Al-Masihi aumbike ndani yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watoto wangu wadogo, ambao nawaonea uchungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watoto wangu, kama vile mama mjamzito anavyotaabika wakati wa kujifungua, mimi nataabika tena kwa ajili yenu mpaka hapo hali yake Kristo itakapoundwa ndani yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watoto wangu, ninao uchungu, kama nitawazaa mara ya pili, mpaka Kristo aonekane kuwa yumo mwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wangu wapendwa, kama vile mwanamuke anavyopata uchungu wa kuzaa, mimi vilevile, ninapata tena uchungu kwa ajili yenu mpaka mutakapokuwa na hali inayokuwa kama ya Kristo ndani yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.