Galatians 4:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: Mmoja kwa mwanamke mtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana imeandikwa kwamba Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja wa mwanamke mtumwa na wa pili wa mwanamke huru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maandiko yanasema kwamba Ibrahimu alikuwa na wana wawili. Mama wa mwana mmoja alikuwa ni mjakazi, na mama wa mwana mwingine alikuwa wa mwanamke aliye huru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mmoja kwa mwanamke mtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mmoja kwa mwanamke mtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wawili, mmoja wa mwanamke mtumwa na wa pili wa mwanamke huru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana imeandikwa kwamba Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja wa mwanamke mtumwa na wa pili wa mwanamke huru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Abrahamu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mwingine kwa mwanamke huru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: Mmoja kwa mwanamke mtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani imeandikwa: Aburahamu alikuwa na wana wawili waume, mmoja wa kijakazi, mmoja wa mkewe mwenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wawili. Alizaa mwana mumoja na muke wake mujakazi na mwingine na muke wake huru wa ndoa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana, imeandikwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.