Galatians 4:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mambo hayo yamekuwa mfano; mama hao wawili ni mfano wa maagano mawili; la kwanza ni lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishi wake ni Hagari, na watoto wake wanazaliwa utumwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza ni lile lililofanyika katika Mlima Sinai, linalozaa watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hajiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Habari hii ina maana nyingine kwenu. Wanawake wawili ni sawa na maagano mawili baina ya Mungu na watu wake. Agano moja ni sheria ambayo Mungu aliifanya katika Mlima Sinai, inayowafanya watu wawe watumwa. Mwanamke aliyeitwa Hajiri yuko kama agano la kwanza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mambo hayo yamekuwa mfano; mama hao wawili ni mfano wa maagano mawili; la kwanza ni lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishi wake ni Hagari, na watoto wake wanazaliwa utumwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mambo hayo yamekuwa mfano; mama hao wawili ni mfano wa maagano mawili; la kwanza ni lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishi wake ni Hagari, na watoto wake wanazaliwa utumwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika mlima wa Sinai, lizaalo watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hagari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika Mlima Sinai, lizaalo watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hagari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mambo hayo yamekuwa mfano; mama hao wawili ni mfano wa maagano mawili; la kwanza ni lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishi wake ni Hagari, na watoto wake wanazaliwa utumwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo hayo yako na maana: kwani wale wanawake wawili ndio maagano mawili. La kwanza ndilo lililotokea mlimani kwa Sinai, linalozaa watumwa tu; hili ndio Hagari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maneno haya ni kama vile mufano: wake hawa wawili ni mufano wa maagano mawili. Yule Hagari, watoto wake waliozaliwa katika hali ya utumwa, ni mufano wa agano lililofanyika kwenye mulima Sinai.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio maagano mawili, moja toka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ndio Hajir.