Galatians 4:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabia, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Hajiri anawakilisha Mlima Sinai ulio Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Hajiri anauwakilisha Mlima Sinai uliopo Arabia. Na anafanana na Yerusalemu wa sasa, kwa sababu mji huu uko utumwani pamoja na watu wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabia, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabia, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabuni na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Hagari anawakilisha Mlima Sinai ulioko Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa yuko utumwani pamoja na watoto wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabia, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana mlima wa Sinai huitwa Hagari kule Arabuni; nao umelingana na Yerusalemu wa sasa, kwani uko utumwani pamoja na watoto wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hagari analinganishwa na mulima Sinai wa inchi ya Arabia, na ni mufano wa Yerusalema ya sasa, unaokuwa katika utumwa pamoja na wakaaji wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana Hajir ni mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemi wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto wake.