Galatians 4:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana imeandikwa: “Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa; paza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto; maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengi kuliko wa yule aliye na mume.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana imeandikwa: “Furahi, ewe mwanamke tasa, wewe usiyezaa; paza sauti, na kuimba kwa furaha, wewe usiyepatwa na uchungu wa kuzaa; kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maandiko yanasema, “Ufurahi mwanamke, wewe uliye tasa. Ufurahi kwani hukuwahi kuzaa. Piga kelele na ulie kwa furaha! Hukupata uchungu wa kuzaa. Mwanamke aliye peke yake atapata watoto zaidi zaidi ya mwanamke aliye na mume.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana imeandikwa: “Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa; paaza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto; maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengi zaidi kuliko wa yule aliye na mume.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana imeandikwa: “Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa; paza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto; maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengi kuliko wa yule aliye na mume.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana imeandikwa: “Furahi, wewe uliye tasa wewe usiyezaa; paza sauti, imba kwa furaha, wewe usiyepatwa na utungu; kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana imeandikwa: “Furahi, ewe mwanamke tasa, wewe usiyezaa; paza sauti, na kuimba kwa furaha, wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa; kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na uchungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana imeandikwa: “Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa; paza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto; maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengi kuliko wa yule aliye na mume.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani imeandikwa: Shangilia, wewe uliye mgumba, usiyezaa! Jichekelee na kupaza sauti, wewe usiyeona uchungu wa kuzaa! Kwani wana wake yule aliye peke yake ni wengi kuliko wana wake yule aliye na mumewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Ufurahi wewe tasa, ushangilie, upige kelele wewe usiyejua uchungu wa kuzaa. Kwa maana muke aliyeachwa na mume, atakuwa na watoto wengi kuliko yule anayekuwa naye.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana imeandikwa, Fanya furaha, tassa usiyezaa; Paaza sauti, ukalie, wewe usiye na utungu; Kwa sababu watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko wake aliye na mume.