Galatians 4:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Maandiko Matakatifu yasemaje? Yasema: “Mfukuze mama mtumwa pamoja na mwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mama huru.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mjakazi na mwanawe! Mwana wa mwanamke aliye huru atapokea kila kitu alicho nacho baba yake, lakini mwana wa mjakazi hatapokea kitu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Maandiko Matakatifu yasemaje? Yasema: “Mfukuze mama mtumwa pamoja na mwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mama huru.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Maandiko Matakatifu yasemaje? Yasema: “Mfukuze mama mtumwa pamoja na mwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mama huru.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Maandiko Matakatifu yasemaje? Yasema: “Mfukuze mama mtumwa pamoja na mwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mama huru.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Maandiko yasemaje? Mfukuze huyu kijakazi pamoja na mwanawe! Kwani mwana wa kijakazi hatapata urithi pamoja na mwana wa mwungwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Maandiko Matakatifu yanasema nini? Yanasema: “Fukuza mujakazi huyu pamoja na mwana wake; kwa maana mwana wa mujakazi hatarizi pamoja na mwana wa muke huru.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini lanenani Andiko? Mtupe nje mjakazi na mwana wake, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.