Galatians 4:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi, wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mwana. Na kwa kuwa wewe ni mwana, Mungu amekufanya wewe pia kuwa mrithi kupitia kwa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa ninyi si watumwa kama mwanzo. Ni watoto wa Mungu, na mtapokea kila kitu ambacho Mungu aliwaahidi watoto wake. Hii yote ni kwa sababu ya yale ambayo Mungu amewatendea ninyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi, wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi, wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mtoto, kwa kuwa wewe ni mtoto, Mungu amekufanya wewe pia kuwa mrithi kwa kupitia Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mtoto, kwa kuwa wewe ni mtoto, Mungu amekufanya wewe pia kuwa mrithi kwa kupitia Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi, wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo hu mtumwa tena, ila umekuwa mwana. Lakini kama umekuwa mwana, umekuwa hata mrithi wa Mungu kwa kuwa wake Kristo.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wewe si mutumwa tena, lakini mwana, na kwa kuwa wewe ni mwana wake, Mungu atakupa sehemu ya urizi aliouahidi kwa wana wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali mwana; na kama u mwana, bassi, u mrithi wa Mungu kwa Kristo.