Galatians 5:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni — awe nani au nani — hakika ataadhibiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nina hakika katika Bwana Isa kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimeridhika moyoni mbele za Bwana kuwa hamtafikiri vinginevyo. Mtu yule anayewasumbua atahukumiwa hata angekuwa nani?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni—awe nani au nani—hakika ataadhibiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni — awe nani au nani — hakika ataadhibiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nina hakika katika Bwana kwa habari yenu kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu awaye yote anayewachanganya anastahili adhabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nina hakika katika Bwana Isa kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewasumbua atachukua hukumu yake, awaye yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni – awe nani au nani – hakika ataadhibiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo, mlivyo naye Bwana, mimi huwawazia kuwa welekevu kwamba: Hamtaigeuza mioyo. Lakini aliyewahangaisha hivyo ataiona hukumu yake, awaye yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa vile mimi niko na tumaini juu yenu kutoka kwa Bwana kwamba hamutakuwa na nia mbalimbali na mimi. Lakini yule anayewavuruga ataazibiwa hata ikiwa ni nani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nina matumaini kwenu katika Bwana, kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anaewafadhaisha atachukua hukumu yake awae yote.