Galatians 5:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaka na dada zangu, sifundishi kuwa ni lazima mwanaume atahiriwe. Kama nitaendelea kuwafundisha wanaume watahiriwe, kwa nini watu bado wanaendelea kunitesa? Ikiwa bado nafundisha tohara, basi ujumbe wangu kuhusu msalaba hautaendelea kuwa tatizo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini basi bado niteswe na Wayahudi? Ukweli kwamba bado wananitesa, ni ushahidi kwamba bado ninahubiri wokovu kupitia msalaba wa Kristo peke yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Kwa kufanya hivyo kikwazo cha msalaba kimeondolewa!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi, ndugu, kama ningetangaza hata sasa, watu watahiriwe, ningekuwa mwenye kufukuzwa? Nayo makwazo ya msalaba yangekuwa yameondolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, ikiwa mimi ningali ninahubiri ya kama ni lazima kutahiriwa, basi kwa sababu gani ningali ninateswa? Kama ningefanya vile, basi watu hawangechukizwa na mahubiri yangu juu ya musalaba wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mimi, ndugu, ikiwa ninakhubiri khabari ya kutahiriwa, mbona ningali nikiudhiwa? Hapo kwazo la msaiaba limebatilika.