Galatians 5:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nasema tena wazi: Kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika sheria yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika Torati yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tena, ninamwonya kila mtu atakayeruhusu atahiriwe, kwamba akifanya hivyo itampasa aifuate sheria yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika Sheria yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika sheria yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nasema tena wazi: Kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika sheria yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena namshuhudia kila mtu aliyetahiriwa, ya kuwa ni mdeni wa kuyafanya Maonyo yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ninasema tena wazi, kila mutu anayekubali kutahiriwa sherti ashike Sheria yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena namshuhudia killa mtu atahiriwae, kwamba ni wajibu wake kuitimiza sharia yote.