Galatians 5:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mnatazamia kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kupitia kwa Torati mmetengwa na Al-Masihi, mko mbali na neema ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa utajaribu kufanyika mwenye haki mbele za Mungu kwa njia ya sheria, maisha yako na Kristo yamepotea, kwani umeiacha neema ya Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mnatazamia kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mnatazamia kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Al-Masihi, mko mbali na neema ya Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mnatazamia kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi mtakao kupata wongofu kwa kuyafanya Maonyo mmetengwa na Kristo, mmeanguka na kuyaacha magawio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama munatafuta kuhesabiwa haki mbele ya Mungu kwa njia ya kushika Sheria, mumejitenga mbali na Kristo na kujipotezea neema ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.