Galatians 5:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kupitia kwa upendo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu anapokuwa wa Kristo Yesu, vyote kutahiriwa ama kutotahiriwa havina nguvu ya kuleta manufaa yoyote. Lakini kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu imani inatenda kazi kupitia upendo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ndani ya Kristo, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana tukiwa naye Kristo Yesu, kunakotupa nguvu siko kutahiriwa, wala kutotahiriwa, ila kumtegemea Mungu kutimilikako katika kupendana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kwa wale wanaoungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakufai kitu. Kitu kinachofaa ni imani inayotenda kazi kwa upendo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.