Galatians 6:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Angalieni herufi kubwa ninazotumia nikiwaandikia kwa mkono wangu mwenyewe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huu ni mwandiko wa mkono wangu mwenyewe. Mnaweza kuona jinsi herufi zilivyo kubwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Angalieni ni herufi gani kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Angalieni herufi kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazameni niandikavyo kwa herufi kubwa niwaandikiapo kwa mkono wangu mimi mwenyewe!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatazameni haya maandiko yote, niliyowaandikia kwa mkono wangu mimi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mujionee wenyewe ni kwa herufi kubwa gani nimewaandikia ninyi kwa mukono wangu mwenyewe!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tazameni kwa harufi gani kubwa nimewaandikieni kwa mkono wangu mimi mwenyewe.