Galatians 6:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha nyinyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: Kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanataka wawalazimishe kutahiriwa. Sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wale wanaojaribu kuwalazimisha ninyi kutahiriwa wanafanya hivyo ili wawaridhishe Wayahudi wenzao. Wanaogopa wasije wakateswa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha ninyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha nyinyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanaotaka wawalazimishe kutahiriwa, sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanataka wawalazimishe kutahiriwa. Sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha nyinyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: Kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote wanaotaka kupendeleza miili, hao huwashurutisha kutahiriwa; tena hapana neno jingine, ni kwamba tu: Wasifukuzwe kwa ajili ya msalaba wake Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu wanaowalazimisha ninyi kutahiriwa, ndio wanaotaka kujionyesha katika mambo yanayoelekea mwili. Lakini wanafanya vile tu kusudi wasiteswe kwa ajili ya kuhubiri habari za musalaba wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mwili, ndio wanaokushurutisheni kutahiriwa: wasiudhiwe tu kwa ajili ya msalaba wa Kristo.