Genesis 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea: mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mungu akasema: Nchi na ichipuze machipuko: mboga ziletazo mbegu na miti ya matunda iletayo matunda, kila mmmoja kwa namna yake, nayo yawe yenye mbegu zao ndani yao za kupandwa katika nchi. Yakawa hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Mungu akasema: “Inchi ioteshe mimea: mimea inayozaa mbegu, na miti inayozaa matunda yenye mbegu za aina yake.” Ikakuwa hivyo.