Genesis 1:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mwenyezi Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nchi ilipotoa machipuko: mboga ziletazo mbegu kwa namna zao na miti iletayo matunda, kila mmoja kwa namna yake, nayo yalikuwa yenye mbegu zao ndani yao, Mungu akayaona kuwa mema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inchi ikaotesha mimea inayozaa mbegu za aina yake, na miti inayozaa matunda yenye mbegu za aina yake. Mungu akaona kwamba ni vizuri.