Genesis 1:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mungu akaumba wanyama wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini, kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mwenyezi Mungu akaona kuwa hili ni jema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu akawaumba nyangumi wakubwa na viumbe vyote wanaokaa majini na kutembea humo, kila mmoja kwa namna yake, nao ndege wote warukao kwa mabawa, kila mmoja kwa namna yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akaumba nyama wakubwa sana wa bahari na aina zote za viumbe vyenye uzima vinavyotembea ndani ya maji. Akaumba aina zote za ndege. Mungu akaona kwamba ni vizuri.