Genesis 1:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: mifugo, viumbe vinavyotambaa ardhini na wanyama pori, kila kiumbe kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwenyezi Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu akasema: Nchi na itoe viumbe vyenye uzima vya kila namna, nyama wa nyumbani na wadudu na nyama wa porini wa kila namna! Yakawa hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akasema: “Inchi itoe aina zote za viumbe vyenye uzima: nyama wa kufugwa, viumbe vinavyotambaa na nyama wa pori wa kila aina.” Ikakuwa hivyo.