Genesis 1:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, mifugo kulingana na aina zake, na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wafugwao kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwenyezi Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mwenyezi Mungu akaona kuwa hili ni jema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo juu ya nchi; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu akawafanya nyama wa porini kila mmoja kwa namna yake na wadudu wote wa nchi kila mmoja kwa namna yake. Mungu akayaona kuwa mema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akafanya aina zote za nyama wa pori, nyama wa kufugwa, na viumbe vinavyotambaa. Mungu akaona kwamba ni vizuri.