Genesis 1:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wanyama wote wa nchi, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
cha wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi. Kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndio chakula chenu; ikawa hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao nyama wote wa nchi na ndege wote wa angani nao wote watambaao katika nchi walio viumbe vyenye uzima, nao chakula chao ni majani yote yanayolika. Yakawa hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao nyama wote katika dunia, ndege wote wa anga, viumbe vyote vinavyotambaa, kila kiumbe chenye uzima, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikakuwa hivyo.