Genesis 11:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tera akawachukua Abramu mwanawe, mjukuu wake Lutu mwana wa Harani, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka Uru ya Wakaldayo pamoja, wakaenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tera akamchukua Abramu mwanawe, Lutu mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Tera akamchukua mwanawe Aburamu na Loti, mwana wa mwanawe Harani, na mkwewe Sarai, mkewe mwanawe Aburamu, wakatoka naye mle Uri wa Wakasidi kwenda katika nchi ya Kanaani, nao walipofika Harani wakakaa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tera akatwaa Abramu mwana wake, Loti mujukuu wake aliyekuwa mwana wa Harani, na Sarai muke wa Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, muji wa Wakaldea, na kwenda katika inchi ya Kanana. Lakini walipofika Harani, wakakaa pale.