Genesis 11:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akasema, “Kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lo lote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akasema: Ninawaona watu hawa kuwa ukoo mmoja tu, nao msemo wao wote ni mmoja tu vilevile. Nao huu ndio mwanzo tu wa matendo yao; sasa yote, watakayoyawaza mioyoni kuyafanya, hakuna lo lote litakalowashinda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akasema: “Watu hawa ni taifa moja na wote wana luga moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayofanya. Jambo lolote wanalokusudia kufanya watafanikiwa.