Genesis 11:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mji huo ukaitwa Babeli, kwa sababu huko ndiko Mwenyezi-Mungu alikoivuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko akawatawanya watu kila mahali duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Mwenyezi Mungu akawatawanya duniani kote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mji huo ukaitwa Babeli, kwa sababu huko ndiko Mwenyezi-Mungu alikoivuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko akawatawanya watu kila mahali duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo BWANA alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo BWANA akawatawanya katika uso wa dunia yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mji huo ukaitwa Babeli, kwa sababu huko ndiko Mwenyezi-Mungu alikoivuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko akawatawanya watu kila mahali duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hiyo wakauita jina lake Babeli (Mvurugo), kwa kuwa huko ndiko, Bwana alikouvuruga msemo wa watu wote wa huku nchini, akawatawanya na kuwatoa huko, wajiendee kukaa katika nchi zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muji ule ukaitwa Babeli, kwa sababu kule ndiko Yawe alikovuruga luga ya dunia yote, na tokea kule akawatawanya watu kila pahali katika dunia.