Genesis 12:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alimchukua Sarai mkewe, na Loti mwana wa ndugu yake, pamoja na mali yao yote na watu wote waliokuwa wamejipatia huko Harani, wakaondoka kuelekea nchi ya Kanaani. Walipoingia nchini Kanaani,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Lutu mwana wa ndugu yake, mali yote waliyokuwa nayo, pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri kwenda nchi ya Kanaani, na wakafika huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alimchukua Sarai mkewe, na Loti mwana wa ndugu yake, pamoja na mali yao yote na watu wote waliokuwa wamejipatia huko Harani, wakaondoka kuelekea nchi ya Kanaani. Walipoingia nchini Kanaani,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Lutu mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alimchukua Sarai mkewe, na Loti mwana wa ndugu yake, pamoja na mali yao yote na watu wote waliokuwa wamejipatia huko Harani, wakaondoka kuelekea nchi ya Kanaani. Walipoingia nchini Kanaani,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aburamu akamchukua mkewe Sarai na Loti, mwana wa nduguye, nayo mapato yao yote, waliyojipatia, nao watu wao wote, waliowapata huko Harani; ndivyo, walivyotoka kwenda katika nchi ya Kanaani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitwaa Sarai muke wake, na Loti mwana wa ndugu yake, pamoja na mali yao yote na watu wote waliokuwa wamejipatia kule Harani, wakaondoka kuelekea inchi ya Kanana. Walipoingia katika inchi ya Kanana,