Genesis 12:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye Abramu akaondoka, akaelekea mlimani mashariki ya Betheli akapiga hema kati ya mji wa Betheli, upande wa magharibi, na mji wa Ai upande wa mashariki. Hapo pia akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu na kumwomba kwa jina lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki mwa Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea Mwenyezi Mungu madhabahu na akaliitia jina la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye Abramu akaondoka, akaelekea mlimani mashariki ya Betheli akapiga hema kati ya mji wa Betheli, upande wa magharibi, na mji wa Ai upande wa mashariki. Hapo pia akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu na kumwomba kwa jina lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea BWANA madhabahu na akaliitia jina la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea bwana madhabahu na akaliitia jina la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye Abramu akaondoka, akaelekea mlimani mashariki ya Betheli akapiga hema kati ya mji wa Betheli, upande wa magharibi, na mji wa Ai upande wa mashariki. Hapo pia akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu na kumwomba kwa jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaondoka huko kwenda kwenye mlima ulioko upande wa maawioni kwa jua kwa Beteli, akalipiga hema lake mahali, Beteli ulipokuwa upande wa baharini nao Ai upande wa maawioni kwa jua; huko akajenga pa kumtambikia Bwana, akalitambikia Jina la Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Abramu akaondoka, akaelekea kwenye mulima upande wa mashariki ya Beteli akapiga hema kati ya muji wa Beteli, upande wa magaribi, na muji wa Ai upande wa mashariki. Pale vilevile akamujengea Yawe mazabahu na kumwomba kwa jina lake.