Genesis 13:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Loti akatazama, akaliona bonde la mto Yordani, akaona kuwa lina maji ya kutosha kila mahali, kama bustani ya Mwenyezi-Mungu na kama nchi ya Misri upande wa Soari. (Hii ilikuwa kabla Mwenyezi-Mungu hajaiangamiza miji ya Sodoma na Gomora).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lutu akatazama, akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya Mwenyezi Mungu, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla Mwenyezi Mungu hajaharibu Sodoma na Gomora.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Loti akatazama, akaliona bonde la mto Yordani, akaona kuwa lina maji ya kutosha kila mahali, kama bustani ya Mwenyezi-Mungu na kama nchi ya Misri upande wa Soari. (Hii ilikuwa kabla Mwenyezi-Mungu hajaiangamiza miji ya Sodoma na Gomora).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Loti akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lutu akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya bwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla bwana hajaharibu Sodoma na Gomora.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Loti akatazama, akaliona bonde la mto Yordani, akaona kuwa lina maji ya kutosha kila mahali, kama bustani ya Mwenyezi-Mungu na kama nchi ya Misri upande wa Soari. (Hii ilikuwa kabla Mwenyezi-Mungu hajaiangamiza miji ya Sodoma na Gomora).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Loti akayainua macho yake, akaliona bonde zima la Yordani, ya kuwa lote lilikuwa lenye maji mengi kufika hata Soari; Bwana alipokuwa hajaiangamiza bado Sodomu na Gomora, lilikuwa kama shamba la Mungu, kama Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Loti akainua macho yake, akaona bonde la muto Yordani, akaona kwamba lina maji ya kutosha kila pahali, kama vile bustani ya Yawe na kama vile inchi ya Misri upande wa Soari. (Hii ilikuwa mbele Yawe hajaiangamiza miji ya Sodoma na Gomora).