Genesis 15:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya mambo hayo, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Abramu katika maono, “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako. Tuzo lako litakuwa kubwa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya jambo hili, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Abramu katika maono, akaambiwa: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya mambo hayo, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Abramu katika maono, “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako. Tuzo lako litakuwa kubwa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu katika maono: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya jambo hili, neno la bwana likamjia Abramu katika maono: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya mambo hayo, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Abramu katika maono, “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako. Tuzo lako litakuwa kubwa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo hayo yalipomalizika neno la Bwana likamjia Aburamu katika ndoto kwamba: Usiogope Aburamu! Mimi ni ngao yako, nao mshahara wako ni mwingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya mambo hayo, neno la Yawe lilimufikia Abramu katika maono kusema hivi: “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako. Zawadi yako itakuwa kubwa!”