Genesis 15:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ujue hakika ya kwamba wazawa wako watakaa kama wageni katika nchi isiyo yao, watakuwa watumwa na watateswa kwa muda wa miaka 400.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni katika nchi isiyo yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ujue hakika ya kwamba wazawa wako watakaa kama wageni katika nchi isiyo yao, watakuwa watumwa na watateswa kwa muda wa miaka 400.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao wenyewe, nao watakuwa watumwa na watateswa kwa miaka mia nne.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yao, watawatumikia watu wale, nao watateswa kwa muda wa miaka mia nne.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ujue hakika ya kwamba wazawa wako watakaa kama wageni katika nchi isiyo yao, watakuwa watumwa na watateswa kwa muda wa miaka 400.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipomwambia Aburamu: Na ujue kabisa, ya kuwa wao wa uzao wako watakaa ugenini katika nchi isiyo yao, nao watawatumikia wenyeji, hao watawatesa miaka 400.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamwambia Abramu: “Ujue hakika kwamba wazao wako watakaa kama wageni katika inchi isiyokuwa yao, watakuwa watumwa na watateswa kwa muda wa miaka mia ine.