Genesis 16:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Wewe ni mjamzito na utajifungua mtoto wa kiume; utamwita Ishmaeli, maana Mwenyezi-Mungu amesikia mateso yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu Mwenyezi Mungu amesikia kuhusu huzuni yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Wewe ni mjamzito na utajifungua mtoto wa kiume; utamwita Ishmaeli, maana Mwenyezi-Mungu amesikia mateso yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia malaika wa BWANA akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu BWANA amesikia juu ya huzuni yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia malaika wa bwana akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu bwana amesikia juu ya huzuni yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Wewe ni mjamzito na utajifungua mtoto wa kiume; utamwita Ishmaeli, maana Mwenyezi-Mungu amesikia mateso yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Malaika wa Bwana akaendelea kumwambia: Ninakuona kuwa mwenye mimba. Mwana, utakayemzaa, mwite jina lake Isimaeli (Mungu husikia), kwa kuwa Bwana amekusikia, ulipomlalamikia kwa kuteseka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha huyo malaika wa Yawe akamwambia: “Wewe una mimba na utazaa mutoto mwanaume; utamwita Isimaeli, maana Yawe ameyaona mateso yako.