Genesis 16:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ishmaeli ataishi kama pundamwitu; atakuwa adui wa kila mtu na kila mtu atakuwa adui yake. Ataishi akiwa adui wa jamaa yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atakuwa kama punda-mwitu kati ya wanadamu; mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu, na mkono wa kila mtu utakuwa dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ishmaeli ataishi kama pundamwitu; atakuwa adui wa kila mtu na kila mtu atakuwa adui yake. Ataishi akiwa adui wa jamaa yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atakuwa kama punda mwitu kati ya watu, mkono wake utapingana na watu wote na mkono wa kila mtu ukipingana naye; na ataishi kwa ugomvi na jamaa yake yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ishmaeli ataishi kama pundamwitu; atakuwa adui wa kila mtu na kila mtu atakuwa adui yake. Ataishi akiwa adui wa jamaa yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atakuwa mwenye ukali kama punda wa porini, mkono wake utawapingia watu wote, nayo mikono yao wote itampingia yeye, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isimaeli ataishi kama punda wa pori. Atapigana na kila mutu na kila mutu atapigana naye. Ataishi peke yake, akijitenga na watu wa jamaa yake.”