Genesis 16:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Hagari akampa jina Mwenyezi-Mungu aliyezungumza naye huko, “Wewe ni Mungu Aonaye” kwa maana alifikiri, “Kweli hapa nimemwona yeye anionaye!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hajiri akampa Mwenyezi Mungu aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Hagari akampa jina Mwenyezi-Mungu aliyezungumza naye huko, “Wewe ni Mungu Aonaye,” kwa maana alifikiri, “Kweli hapa nimemwona yeye anionaye!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akampa BWANA aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hagari akampa bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akampa jina BWANA aliyesema naye, “Wewe U Mungu uonaye,” kwani alisema, “Kweli nimemwona Mungu na nikaendelea kuishi baada ya kumuona?”
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Hagari akampa jina Mwenyezi-Mungu aliyezungumza naye huko, “Wewe ni Mungu Aonaye” kwa maana alifikiri, “Kweli hapa nimemwona yeye anionaye!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipomwita Bwana aliyesema naye jina lake: Wewe Mungu unaniona, kwani alisema: Kumbe nami nimemwona, aliponitazama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaliita jina la BWANA aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Hagari akamupa Yawe aliyezungumuza naye kule jina la “Wewe ni Mungu Anayeona,” kwa maana alifikiri: “Kweli hapa nimemwona yeye anayeniona?”