Genesis 16:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Mwenyezi Mungu amenizuilia kupata watoto. Basi nenda ukutane kimwili na mjakazi wangu; huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hivyo Sarai akamwambia Abramu, “BWANA amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hivyo Sarai akamwambia Abramu, “ bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sarai akamwambia Abramu, kwa kuwa BWANA amenifunga tumbo nisizae, sasa mwingilie mjakazi wangu, labda nitapata uzao kutoka kwake. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo akamwambia Aburamu: Unaona, ya kuwa Bwana amenifunga, nisizae; sasa ingia kwa kijakazi wangu! Labda nitapata mlango kwake yeye. Aburamu akayaitikia, Sarai aliyoyasemaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Sarai akamwambia Abramu: “Unajua kwamba Yawe hajanijalia kupata watoto. Umutwae Hagari mujakazi wangu. Labda nitapata watoto kutoka kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.