Genesis 16:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Sarai akampa Abramu Hagari, mjakazi wake ambaye alikuwa Mmisri, awe mke wake. Haya yalitokea baada ya Abramu kukaa katika nchi ya Kanaani kwa muda wa miaka kumi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mjakazi wake Mmisri aliyeitwa Hajiri, na kumpa mumewe awe mke wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Sarai akampa Abramu Hagari, mjakazi wake ambaye alikuwa Mmisri, awe mke wake. Haya yalitokea baada ya Abramu kukaa katika nchi ya Kanaani kwa muda wa miaka kumi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo, baada ya Abramu kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani, Sarai mkewe Abramu alimtwaa Hajiri Mmisri, mjakazi wake, akampa Abramu mumewe, kama mke.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Sarai akampa Abramu Hagari, mjakazi wake ambaye alikuwa Mmisri, awe mke wake. Haya yalitokea baada ya Abramu kukaa katika nchi ya Kanaani kwa muda wa miaka kumi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Sari, mkewe Aburamu, akamchukua Hagari, kijakazi wake wa Kimisri, akampa mumewe Aburamu kuwa mkewe, Aburamu naye alikuwa amekwisha kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Sarai akamupa Abramu Hagari, mujakazi wake Mumisri, akuwe muke wake. Haya yalitokea nyuma ya Abramu kukaa katika inchi ya Kanana kwa muda wa miaka kumi.