Genesis 16:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sarai akamwambia Abramu, “Wewe utawajibika kwa ubaya ninaotendewa. Mimi nilikupa mjakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake! Mwenyezi-Mungu na ahukumu kati yako na mimi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na mateso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mkononi mwako. Sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Mwenyezi Mungu na aamue kati yako na mimi!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sarai akamwambia Abramu, “Wewe utawajibika kwa ubaya ninaotendewa. Mimi nilikupa mjakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake! Mwenyezi-Mungu na ahukumu kati yako na mimi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. BWANA na aamue kati yako na mimi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. bwana na aamue kati yako na mimi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sarai akamwambia Abramu, “Wewe utawajibika kwa ubaya ninaotendewa. Mimi nilikupa mjakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake! Mwenyezi-Mungu na ahukumu kati yako na mimi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Sarai alipomwambia Aburamu: Mabaya ninayofanyiziwa na yakujie wewe! Mimi nimemweka kijakazi wangu kifuani pako; naye alipojiona kuwa mwenye mimba hunibeua, niwe mdogo machoni pake. Bwana na atuamulie mimi na wewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sarai akamwambia Abramu: “Lazima ya ubaya ninaotendewa ikuwe juu yako. Mimi nilikupa mujakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa kitu bure mbele ya macho yake! Yawe ahukumu kati yako na mimi!”