Genesis 17:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mtoto wa kiume wa siku nane miongoni mwenu ni lazima atahiriwe. Kila mwanamume katika vizazi vyenu, awe mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwenu au aliyenunuliwa kwa fedha zenu kutoka kwa mgeni asiye mzawa wako;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio wa uzao wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mtoto wa kiume wa siku nane miongoni mwenu ni lazima atahiriwe. Kila mwanamume katika vizazi vyenu, awe mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwenu au aliyenunuliwa kwa fedha zenu kutoka kwa mgeni asiye mzawa wako;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mtoto wa kiume wa siku nane miongoni mwenu ni lazima atahiriwe. Kila mwanamume katika vizazi vyenu, awe mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwenu au aliyenunuliwa kwa fedha zenu kutoka kwa mgeni asiye mzawa wako;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwenu kila mtoto wa kiume aliye wa vizazi vyenu akimaliza siku nane sharti atahiriwe. Vivyo hivyo nao wazalia wa nyumbani nao wasio wa uzao wako walionunuliwa kwa fedha kwa wageni wo wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mutoto mwanaume kati yenu anapaswa kutahiriwa kwa umri wa siku nane. Vilevile watumwa waliozaliwa katika nyumba yenu au walionunuliwa kwa feza zenu kutoka kwa wageni wasiokuwa wa uzao wenu. Hiki ni kitambulisho cha agano langu katika miili yenu, agano la milele.