Genesis 17:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na, kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Nitambariki, nitamjalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Ishmaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya kuwa baba wa taifa kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu Ishmaeli, nimekusikia. Hakika nitambariki; nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na, kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Nitambariki, nitamjalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Ishmaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya kuwa baba wa taifa kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu Ishmaeli nimekusikia, nimembariki na nitamzidisha na kumwongeza sana. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, na atakuwa na taifa kuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Na, kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Nitambariki, nitamjalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Ishmaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya kuwa baba wa taifa kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata kwa ajili ya Isimaeli nimekusikia: Tazama, nitambariki naye na kumpa wazao wengi na kumfanya kuwa wengi sanasana, atazaa wakuu 12, nami nitamfanya kuwa taifa kubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Na juu ya Isimaeli, nimesikia ombi lako. Nitamubariki, nitamujalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Isimaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamufanya kuwa baba wa taifa kubwa.