Genesis 17:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele; tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitalithibitisha agano langu kama agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo, nami nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele; tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele; tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitalisimamisha agano langu, tuliloliagana mimi na wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako, liwe agano la vizazi vya kale na kale, niwe Mungu wako na Mungu wao wa uzao wako wajao nyuma yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Nitasimamisha agano langu nawe, wazao wako na vizazi vyao vyote milele; nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazao wako milele.