Genesis 17:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambamo unaishi kama mgeni; yaani nchi yote ya Kanaani iwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi yote ya Kanaani, unayoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na ya uzao wako; nami nitakuwa Mungu wao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambamo unaishi kama mgeni; yaani nchi yote ya Kanaani iwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayokaa kama mgeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambamo unaishi kama mgeni; yaani nchi yote ya Kanaani iwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitakupa wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako nchi hii, unayoikaa ugeni, ndiyo nchi yote ya Kanaani, mwichukue, iwe yenu kale na kale, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakupa wewe na wazao wako inchi hii ambamo unaishi kama mugeni. Ni kusema inchi yote ya Kanana ikuwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”