Genesis 18:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Hakika nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, na Sara mkeo atakuwa na mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema lililokuwa nyuma ya Ibrahimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Nitakaporudi kwako siku zizi hizi za mwaka ujao, ndipo, mkeo Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume. Naye Sara aliyasikia, maana alikuwa nyuma yake hapo pa kuingia hemani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumoja wao akasema: “Hakika nitakurudilia kwa wakati kama huu katika mwaka na muke wako Sara atakuwa na mutoto mwanaume.” Sara alikuwa kule nyuma kwenye mulango wa hema, akisikiliza.